Jun 19, 2012

Posted by Dismas Ten Tuesday, June 19, 2012 No comments
Baada ya Twiga Stars kushindwa kufuzu kuelekea katika fainali za mataifa ya Afrika nchini Equtorial Guinea baadaye mwaka huu, timu za Taifa za wanawake za Nigeria, Cameroon, Cote d’Ivoire, Ethiopia, South Africa, DR Congo na Equatorial Guinea zimefuzu fainali hizo zitakazo pigwa nchini Equtorial Guinea.

Timu ya taifa ya wanawake wa Nigeria (Super Falcons) imefuzu fainali za mataifa ya Afrika kwa wanawake 2012 baada ya kuwachapa Zimbabwe 4-0 katika mchezo wa pili wa kuwania kufuzu mchezo ulipigwa Lagos jumamosi.

Super Falcons imefanikiwa ikiwa kaida yao kufanya hivyo tangu kuanzishwa mwaka 1998 kwa ushindi wa jumla wa mabao 6-0.
Mabingwa hao watetezi walikuwa ni zaidi mara dufu kimchezo mbele ya Mighty Warriors na kuthibitisha hadhi yao wakiongoza mpaka kipindi cha kwanza kwa mabao matatu.

Ndani ya dakika sita mchezaji bora wa mwaka Perpetua Nkwocha alifunga bao la uongozi kwa shambulizi zuri kabla ya Desire Oparanozie kuongeza la pili dakika 14 baadaye.
Dakika mbili baadaye Esther Sunday akaongeza la tatu licha ya juhudi za mlinda mlango wa Zimbabwe Onai Chingowo kujaribu kuokoa mpira huo.

Kiungo mkongwe Stella Mbachu alimalizia karamu kwa goli la nne kunako dakika ya 55 ya mchezo.

0 COMMENTS:

TAFUTA HAPA

UNGANA NASI

Delicious Digg Facebook Favorites More Stumbleupon Twitter