Jun 11, 2012

Posted by Dismas Ten Monday, June 11, 2012 No comments
 Mlinzi wa  pembeni wa timu ya taifa ya  Tanzania  Erasto  nyoni amesema  kuwa  aliamini  atafunga  mkwaju wa  penati  iliyopata  timu ya  taifa ya Tanzania  Taifa  Stars kufuatia  mlinzi wa  timu ya Gambia  kuunawa mpira  kwenye eneo la hatari.

Mara baada  ya kumalizika kwa  mchezo huo Erasto  aliiambia  Blog hii  kuwa, aliingiwa  na furaha ya ajabu baada ya nahodha  Juma  Kaseja  kumwambia  nakuamini nenda  kapige penati hiyo nina  imani utafunga  na kuwapa raha Watanzania.

"Nilifurahi Kaseja  aliponiteua kupiga penati na kwa  kuwa  sina kawaida ya kukosa  niliamini  nitafunga penati hiyo  na kuwapa Watanzania  kile walichokuwa wanakisubiri, kwa  kweli  nimefurahi sana na  zaidi  nimefurahi  kuona  mashabiki wote  uwanjani wameondoka na furaha  baada ya timu kupata  ushindi"  alisema  Nyoni.

0 COMMENTS:

TAFUTA HAPA

UNGANA NASI

Delicious Digg Facebook Favorites More Stumbleupon Twitter