Jun 17, 2012

Posted by Dismas Ten Sunday, June 17, 2012 No comments
Kocha mkuu wa timu ya soka ya taifa ya wanawake Charles Boniface Mkwasa amesema hawezi kuwatupia lawama wachezaji wake kufuatia kipigo cha bao 1-0 walichokipata kwenye mchezo wa pili kuwania kufuzu kwa fainali za mataifa Afrika kwa wanawake uliopigwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Blog hii mapema Leo mkwasa amesema kuwa kilichotokea ni hali ya mchezo huku akisisitiza kuwa kuwa huu siyo tena wakati wa kutupiana lawama na kutafuta mchawi kilichobaki ni kujipanga kwa mashindano mengine yatakayofuata siku za usoni.

"Si jambo jema kuwalaum wachezaji kwa kilichotokea, ni jambo linalouma kuona tumeshindwa kufuzu wakati tulihitaji bao moja tu kukata tiketi, huo ndoio mchezo wa soka sitaki kutupa lawama kwa yoyote, kilichobaki ni kujipaga kwa michuno mingine itakayofuata hapoa baadae" alisema Mkwasa kwa masikitiko makubwa

0 COMMENTS:

TAFUTA HAPA

UNGANA NASI

Delicious Digg Facebook Favorites More Stumbleupon Twitter