Jun 16, 2012

Posted by Dismas Ten Saturday, June 16, 2012 No comments
Wakati timu ya taifa ya wanawake ikitarajia kushuka dimbani kucheza mchezo wa marudiano dhidi ya akina dada wa Ethiopia ukiwa ni mchezo wa kuwania kufuzu kucheza fainali za matiafa ya Afrika fainali ambazo tichezwa nchini Equatorial Guinea, dua na sala za watanzania zinapaswa kuongezeka ili timu hiyo itimize azma hiyo.

Twiga watashuka dimbani jioni ya leo kuwakabili wahabeshi hao huku ikiwa na deni la kufungwa katika nchini mchezo wa kwanza ulifanyika nchini Ethiopia kwa bao 2-1 na hivyo inahitaji kupata ushindi angalau wa bao 1-0 ilikuweza kusonga mbele.

Hata hivyo Twiga watalazimika kucheza kwa tahadhari kubwa kulinda lango lisiruhusu goli kwa wahabeshi ambalo linaweza kuuweka mchezo huo katika hali ngumu zaidi kwani kwa kuruhusu bao hata moja kutawafanya akida wa Twiga kupata kazi kubwa na ya ziada ya kupata mabao mengi zaidi ili kuwaondosha Ethiopia mashindanoni.

Ethiopia wanaotumia jina la kiutani kama "LUCY"wanaofundishwa na kocha Abrham Teklehaimanot na ambao wanamtegemea zaidi mshambuliaji wao hatari Birtukan na Gebrekirstos ambao wamenukuliwa na sokaletutz wakijigamba kuwa wanajua mazingira ya mchezo yanayo wakabili na hivyo wako tayari kupigana kufa kupona kulinda goli lao moja la uongozi walilolipata nyumbani kwao Ethiopia.

Kwa watanzania ni kuongeza dua zao ili Twiga kupata ushindi.

0 COMMENTS:

TAFUTA HAPA

UNGANA NASI

Delicious Digg Facebook Favorites More Stumbleupon Twitter