Jun 16, 2012

Posted by Dismas Ten Saturday, June 16, 2012 No comments
Baraza la vya vya soka Afrika mashariki na kati (CECAFA) limetangaza tarehe ya kuanza michuano ya Kagame michuano ambayo ushindanisha vilabu bingwa katika ukanda wa huu.

Akizungumza na waandishi wa habari hii leo Rais wa baraza hilo ambaye pia ni Rais shirikisho la soka la Tanzania leordigar Chila Tenga amesema michuano hiyo italazimika kufanyika ili kuokoa heshima ya ukanda huu ambao kisoka ni mkubwa na una heshima kubwa barani Afrika na duniani kwa ujumla kutokana na historia yake.

Tenga amesema cecafa imekuwa ikifanya jitihada kubwa kuwapata wadhamini wa michuano hiyo kufuatia muda wa udhamini wa kampuni ya Tusker ambao ni watengenezaji wa vinywaji vya pombe kudhamini michuano hiyo kwa mwaka mmoja yaani mwaka jana.

Tenga amesema kimsingi wajumbe wa kamati ya utendaji ya CECAFA walikutana wakati wa mkutano wa shirikisho la soka barani afrika CAF ndipo walipokubaliana kuwa michuano hiyo ifanyike licha ya kutokuwepo kwa udhamni mpaka wakati huo huku jitihada za kusaka wadhamini wengine zikiendelea.

Hata hivyo Rais Tenga amesema wanaimani huenda michuano hiyo ikapata wadhamni mbalimbali kwani michuano hiyo itaonyeshwa moja kwa moja na kituo cha television cha Super Sport pamoja na baadhi ya vituo vya television vya Tanzania.

Michuano hiyo imepangwa kuanza kutimua vumbi Julai14-29 jijini Dar es Saalam huku Tanzania ikiingiza timu tatu za Yanga ambao ni mabingwa watetezi, Simba mabingwa wapya wa Tanzania bara na Azam fc kama washindi wa pili wa ligi ya Tanzania bara wakitumia faida ya nchi mwenyeji kuingiza timu mbili.

Akitangaza tarehe hiyo ya kuanza kwa michuano, katibu mkuu wa baraza hilo Nickolaus Musonye amesema michuano hiyo itaanza tarehe hiyo jijini Dar es Saalam lakini huku akivitaka vilabu shiriki kuthitisha mapema kabla ya tarehe ya mwisho ya kuthibitsha ambayo ni tarehe 25/06/2012.

Musonye amesema tayari CECAFA imepokea maombi toka vilabu mbalimbali barani Afrika vikiomba kushiriki michuano hiyo kama vilabu alikwa vikiwemo vilabu vya Platinum ya Afrika kusini na vilabu vingine viwili toka nchini humo.

klabu nyinvine Vita club ya DRC Congo na timu mbili toka nchini Zimbabwe moja ikiwa ni Dynamos. Aidha amesema maombi hayo yatategemea uthibitisho wa vilabu toka ukanda wa CECAFA na kama kutakuwa na klabu ambayo haikuthibitisha ndipo timu ambazo zimeomba nje ya nchi wanachama wa Afrika mashariki watafikiriwa kuingia mashindanoni.

0 COMMENTS:

TAFUTA HAPA

UNGANA NASI

Delicious Digg Facebook Favorites More Stumbleupon Twitter