Jun 11, 2012

Posted by Dismas Ten Monday, June 11, 2012 No comments

 Msafara wa mabasi zaidi ya 50 unatarajia kulisimamisha  jiji la Dar es Salaam wakati wa mapokezi ya kocha Macio Maximo anayetarajiwa  kutua nchini wakati wowote tayari kujiunga na Yanga.

Akizungumza na  Blog mapema leo hii mmoja wa mashabiki wa timu hiyo ya mtaa wa jangwani  amesema kuwa mabasi zaidi 50 ya kukodi yametolewa na mmoja wagombea uongozi  katika uchaguzi mkuu wa timu hiyo  kwa heshima ya kocha huyo aliyekubari kujiunga  na timu yao

“Nakuambia  ukweli  mabasi zaidi ya 50  mwenyewe  nimeshuhudia wakilipwa pesa zao kwa ajili ya  kazi hiyo ya kumpokea Maximo nina uhakika  yatakuwa mapokezi ya aina  yake ambayo hayajawahi kutokea nchini”  alisema Shabiki huyo anayewakilisha  kundi la Yanga Bomba.

0 COMMENTS:

TAFUTA HAPA

UNGANA NASI

Delicious Digg Facebook Favorites More Stumbleupon Twitter