Jul 5, 2012

Posted by Dismas Ten Thursday, July 05, 2012 No comments


Tom Saintfiet amezaliwa March 29 mwaka 1973 huko Mol nchini Belgium.
Ni meneja wa chama cha soka nchini Meneja na mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Belgium. alikuwa ni mchezaji wa soka kati ya mwaka 1983 na 1997 kabla ya kuwa meneja akiwa na umri wa miaka 24 akiwa ni meneja mdogo kuwahi kutokea nchini Belgium.
Saintfiet amefundisha soka katika mataifa mbalimbali ikiwemo Belgium, Qatar,Ujerumani Germany,visiwa vya Faroe, Finland na uholanzi . Pia amefanya kazi barani Afrika ambapo amekuwa kocha mkuu wa timu ya taifa za Namibia na Zimbabwe. kabla ya kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa Namibia, Saintfiet alikuwa meneja wa timu ya ligi kuu ya nchini Finland ya RoPS Rovaniemi. Mwaka 2002Tom Saintfiet ameifundisha timu moja ya visiwa vya Faroe ya B71 ambayo ilimaliza ligi katika nafasi ya pili katika ligi ya nchi hiyo mwaka huo.
baadaye akaelekea kuifundisha Al-Ittihad Sports Club ya nchini Qatar ambayo sasa inatambulika kama Al-Gharafa Sports Club. mwaka 2004 alipata nafasi ya kuifundisha timu ya taifa ya vijana( chini ya miaka 17) ya nchini Qatar ambayo ilifanikiwa kushika nafasi ya tatu katika vijana barani Asia na kufuzu kucheza fainali za vijana za shirikisho la soka dunaini FIFA kwa wachezaji wenye umri huo(17 FIFA World Championships).
Kuelekea katika fainali za kombe la dunia mwaka 2010 (FIFA World Cup 2010) , Saintfiet alikuwa ni miongozi mwa makocha waliopendekezwa na shirikisho la soka nchini Nigeria kuifundisha timu ya taifa hilo maarufu Super Eagles fainali ambazo baadaye zilifanyika nchini Afrika kusini.
Namibia
Saintfiet alianza kuifundisha timu ya taifa ya Namibia kwa mafanikio akipata ushindi dhidi ya Comoros na timu ya taifa ya Malawi(The Flames) kisha kupata sare dhidi ya Lesotho katika michuano ya Cosafa maarufu kama ‘Cosafa Senior Challenge Cup’ nchini Afrika kusini July 2008.
Namibia iliondoshwa katika robo fainali na waliokuwa wenyeji Afrika kusini(BafanaBafana). Mafanikio ya Saintfiet ni pamoja na ushindi wa mabao 4-2 mwaka 2010 mchezo wa kuwania kufuzu kombe la dunia pamoja na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Congo DR mchezo wa kirafiki.
Siku tatu baada ya sare ya bao 1-1 ugenini dhidi ya Lebanon April 2009, Namibia kwa mara nyingine tena ilipata sare nyingine ya 0-0 ugenini dhidi ya Angola.
matokeo mengine ya mafanikio Arguably his most ni kule mjini Durban,pale Namibia ilipokwenda sare ya bao 1-1 dhidi ya Afrika Kuisni.
Namibia ilikuwa imeshinda mchezo mmoja tu kabla ya Saintfiet kuwasili nchini humo katika jumla ya michezo 12 iliyocheza.
Baada ya mafanikio hayo vyombo vya habari vilianza kumwita kwa jina la utani "The Saint" na huku gazeti moja likimwita "The Messiah".
Zimbabwe
baada ya kuwepo na taarifa zilizo muhusisha na kazi nchini Zimbabwe , Sainfiet akafanikiwa miongoni mwa makocha 15 waliomba kazi nchini humo kupata kazi hiyo na kusaini mkataba wa miaka 4 na shirikisho la soka la nchi hiyo ZIFA October 2010.
Mwezi November, mamlaka ya uhamiaji nchini Zimbabwean ilikataa kutoa kibali cha kazi kumruhusu kocha huyo wa Warriors Saintfiet ambaye baada ya ZIFA ililazimika kusaka kibali cha muda.
October 10 Zimbabwe ilicheza na Cape Verde mjini Harare mchezo wa kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Afrika 2012 na kwenda sare ya bao 1-1. Sainfiet aliendelea kutoa mafunzo kwa timu yake licha ya kuambiwa kuondoka katika kambi ya timu hiyo kutokana na kukosa kibali cha kufanya kazi nchini humo.
Akiwa nchini Namibia alikokuwa akiishi , Saintfiet, alitengeneza mipango yake ya kiufundi kwa ajili ya timu ya taifa ya Zimbabwe na kutaja kikosi cha timu ya taifa ambacho kiliichapa Mozambique mabao 3-1 katika mchezo uliofuata.
Baada ya maombi ya kibali cha kazi kushindikana basi ikalazimika Saintfiet kuachana na kazi ya kuifundisha timu ya taifa ya Zimbabwe December 2010.
Shabab Al Ordon
Mwishoni mwa December 2010, Tom alisaini mkataba wa miezi 4 Month na mabingwa wa mwaka 2007 wa taji la AFC Cup, Shabab Al Ordon.
Kwa mara nyingine tena alifanikiwa kusuka eneo la ulinzi la timu hiyo ambayo iliruhusu bao moja katika jumla ya michezo mitano na Saintfiet akiwa kocha mkuu. Baada ya michezo sita alipata matokeo ya ushindi katika michezo mitatu na sare tatu. Kutokana na matatizo ya mahitaji yake kutokutimizwa kama ilivyo tatikana aliamua kuondoka Shabab Al Ordon baada ya kuifikisha katika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi bila ya kufungwa.
Ethiopia
Baada ya maombi ya timu tatu za taifa , Saintfiet alitajwa kama kocha mkuu wa timu ya taifa ya Ethiopia May 2011. Mkataba wa muda mfupi ulikubaliwa na Saintfiet alianza mchezo wake wa kwanza siku kumi baadaye.
Ethiopia kuelekea katika mchezo dhidi ya Nigeria kampeni ya kucheza mataifa ya Afrika 2012, ililazimika kucheza dhidi ya Argentina ambapo ilifungwa mabao 4-1 siku nne kabla ya mchezo huo na baadaye ikaichapa Ethiopia 4-0 katika mchezo wa kufuzu AFCON nchini Nigeria mbele ya watazamaji 30,000 ambao walikuwa wakitazama mchezo wa kwanza wa Saintfiet na kuridhishwa na kiwango cha Ethiopia ambao mpaka mapumziko walikuwa sare ya bao 1-1.
Baada ya mchezo kocha wa Nigeria Samson Siasia alikaririwa akisema ameshangazwa hali ya nidhamu ya mchezo ilionyeshwa na Ethiopia. Pamoja na mafaniko yake yote bado Thom aliamua mwenyewe kujiuzulu ukocha October 28 2011.

Nigeria
March 28 2012 kocha huyo raia wa Belgium Tom Saintfiet alipewa mkataba wa miaka minne kama mkurugenzi wa ufundi wa shirikisho la soka la nchini Nigeria ,hata hivyo mkataba wake ulivunjwa mwezi June.

Sifa Binafsi
Saintfiet ana leseni ya UEFA Pro Licence, ambayo aliipata mwaka 2000.
Kati ya 2006 2007 alikuwa ni mkurugenzi wa ufundi wa FC Emmen (ligi daraja la kwanza ya Uholanzi) na pia alifanya kazi kama mshauri wa soka katika shirikisho la soka la Kazakhstan.
Alifanyakazi pia kama mchambuzi wa mpira wa miguu katika Television za kuonyesha mpira wa miguu za nchi za Belgium , Afrika kusini na Namibian pia kama mkalimani wa DFB. amesomea mambo saikolojia katika michezo na saikolojia ya uchumi.
Saintfiet anazungumza lugha nyingi ikiwemo kidachi, Kingereza, kifaransa, kijerumani, lugha ya Faroese na ana uwelewa kiasi katika lugha za kiarabu , kiafrikana na kispanish.
Ni mwandishi mzuri pia wa makala . Katika fainali ya kombe la dunia za FIFA mwaka 2010, Saintfiet aliandika makala kwa ajili ya vyombo vya habari vya nchini Belgium (Sport/Voetbal Magazine) na vile vya nchini Japan.

0 COMMENTS:

TAFUTA HAPA

UNGANA NASI

Delicious Digg Facebook Favorites More Stumbleupon Twitter