Jul 5, 2012

Posted by Dismas Ten Thursday, July 05, 2012 No comments
BEKI wa Simba SC, Juma Said Nyosso (pichani kushoto)amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuendelea kuichezea klabu hiyo, baada ya mkataba wake awali kumalizika, hivyo kumaliza tetesi kwamba anaweza kuhamia kwa watani wa jadi, Yanga SC.
Makamu Mwenyekiti wa Simba SC, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ amesema kuwa Nyosso alisaini mkataba huo Julai 1, mwaka huu.

Kaburu alisema kwamba Simba ina imani na beki huyo wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars na ndio maana imemuongezea mkataba.
Aidha, Kaburu aligusia suala la beki wao, Kelvin Yondan aliyehamia kwa watani wa jadi, Yanga akisema kwamba bado ni mchezaji wao halali na wamekwishapeleka malalamiko yao Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), wanasubiri majibu.

Kaburu pia amesema mshambuliaji wa kimataifa wa Zambia, Felix Sunzu tayari amejiunga na wenzake kambini visiwani Zanzibar, ambako timu hiyo inashiriki Kombe la Urafiki.

Kaburu amesema Simba itaendelea kuwa Zanzibar hata baada ya michuano hiyo, wakijiandaa na Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, ambalo linatarajiwa kuanza kutimua vumbi Julai 14, Simba wakifungua dimba na URA ya Uganda Julai 16.

0 COMMENTS:

TAFUTA HAPA

UNGANA NASI

Delicious Digg Facebook Favorites More Stumbleupon Twitter