Dec 23, 2010

Posted by Dismas Ten in | Thursday, December 23, 2010 1 comment
STEVEN CHARLES KANUMBA
Msanii ‘matawi ya juu’ katika kiwanda cha filamu Bongo Steven Kanumba ‘The Great’ ameibuka na kukanusha vikali stori zilizoenea kitaa kuwa yeye na waaandaaji wengine wa filamu wakemuwa wakiwakimbilia mamiss, na kuwajumuisha kuigiza muvi kwa lengo la kuongeza kipato ilihali wakijua kwamba warembo hao hawana uwezo wa kuigiza.

Kanumba, ambaye hivi sasa anamiliki kampuni yake binafsi ya filamu inayokwenda kwa jina la Kanumba Film Production, alisema hayo wiki aliyopita katika mahojiano maalum na www.dismasten.blogspot.com, kufuatia kuwepo kwa malalamiko mengi ya wapenzi wa filamu juu ya kutumiwa kwa wasichana wenye umaarufu fulani wakati uwezo wao wa kuigiza ni mdogo.

“Ndiyo ni kweli tumesikia juu ya malalamiko, lakini mimi binafsi sijawahi kumuita wala kumtafuta miss ama msichana yoyote maarufu kwa ajili ya kazi isipokuwa wao ndiyo wamekuwa wakitupigia simu na kuomba tuwape kazi hiyo” alisema kanumba

Akiendelea zaidi msanii huyo ambaye kwa mara ya kwanza Muvi yake ya ‘Black Sunday’ imeonyeshwa kwenye majumba ya Sinema hapa nchini alianika kuwa kumekuwa na ugumu fulani katika kuwagundua wasanii wengine wenye vipaji ndiyo maana wamekuwa wakiamua kuwapa nafasi mamis wanaoomba kufanya kazi hiyo kwa kuwa wanapatikana kirahisi

“Nikiwa kama muandaaji wa filamu kuna sifa kama tano hivi ambazo mwigizaji anatakiwa awe nazo ili kupewa nafasi hiyo sasa inakuwa shida kidogo kwa wasichana wa mtaanii kuzikamilisha hii inatufanya kuwa na wakati mgumu sana wa kuwatafuta” alisema

Alipoulizwa aina ya sifa hizo Kanumba alizitaja kuwa ni pamoja na Uzuri wa sura, Umbo, kimo, elimu kwa maana ya kujua lugha tofauti, kutembea (Motion) na pia kujiamini.

Katika hatua nyingine nyota huyo anayesumbua sokoni na muvi yake ya ‘More than Pain’ aliwataka wasichana wanaoona kuwa wana uwezo na sifa za kuigiza, kukaa tayari kwani kuna mpango maalum ambao ameundaa kwa ajiri ya kutafuta vipaji vya wasichana kutoka mtaani

1 COMMENTS:

Anonymous said...

acha uongo wewe ni mwizi kila mtu anajua

TAFUTA HAPA

UNGANA NASI

Delicious Digg Facebook Favorites More Stumbleupon Twitter