Dec 23, 2010

Posted by Dismas Ten in | Thursday, December 23, 2010 1 comment
Shilole akiwa 'bize' na kutafuna Kiti Moto's
PAMOJA na kuwa ni muumini wa dini ya Kiislamu, nyota kutoka kiwanda cha filamu Bongo Zuwena Mohamed ‘Shilole’ juzikati alinaswa akibugia ‘Kiti moto’ (nyama ya nguruwe) mchana kweupe bila wasiwasi wowote. Tukio la nyota huyo kunaswa akila nyama hiyo iliyopewa alama X katika vitabu vya Mwenyezi Mungu, lilitokea Jumatano ya wiki hii katika Baa maarufu ya Panama iliyopo maeneo ya Kinondoni Studio jijini Dar es Salaam.
Dakika chache baada ya kumaliza ‘kufakamia’ haramu hiyo Shilole alifunguka kuwa hafahamu lolote kama kula Kiti Moto ni haramu kwani tangu ameanza kula nyama hiyo hajawahi kuvimba miguu wala kushindwa kutembea kwa hiyo anahisi hana kosa lolote kula kile ambacho moyo wake unapenda. “Kila mtu anao huru wa kufanya kile anacho kipenda sharti tu asivunje sheria za nchi na katika sheria za Bongo hakuna sehemu iliyoandikwa Watanzania marufuku kula Kiti moto ndiyo maana mimi na kula kwa sababu naizimia sana na sijawahi kupata tatizo lolote toka nimeanza kutafuna nyama hii ” alisema Shilole. Katika hatu nyingine nyota huyo wa filamu ya ‘Dar es Salaam Sister’ alienda mbali zaidi na kusema katika ulimwengu huu si watu wote watakaouona Ufalme wa Mungu, na kama kula Kiti Moto ni dhambi kubwa basi duniani hakuna atakaye pona kwani hata hao wanaojiita wenye dini nao wana kula nyama hiyo. “Kuna watu hapa duniani wanafanya mambo ya ajabu kuliko hata hili la mimi kula Kiti Moto lakini hayasemwi na kama kula nyama hii ndiyo zambi kubwa basi hakuna atakayepona, hebu jiulize na wewe kiongozi wa dini aliyeoa shoga ama kiongozi fulani anayechukua mke wa mtu na mimi ninayekula Kiti Moto nani ananafuu ? alimaliza Shilole kwa kwa kuhoji.



1 COMMENTS:

Anonymous said...

jinga tu halina lolote likafanye ukahaba tu...

TAFUTA HAPA

UNGANA NASI

Delicious Digg Facebook Favorites More Stumbleupon Twitter