
Akizungumza na SLT mapema jana kocha huyo raia wa Serbia amesema kuwa majeruhi wengi waliopo katika timu hiyo na pia wachezaji kutokutumia vyeama mafundisho yake ni moja ya sababu zinazompa wasiwasi mkubwa wa kufanya vizuri dhidi ya miamaba hiyo ya Misri.
"Tuna majeruhi wengi, lakini wachezaji wangu hawaonekani kufanya yale ninayowafundisha tukiwa mazoezini hakika hili linanipa shaka kwani Zamalek ni timu bora Afrika na kila mmoja wetu anafahamu juu ya hilo, kwa sasa sina imani kama tunaweza kufanya vizuri licha ya kuwa tunacheza nyumbani" alisema Papic.
Siku chache zilizopita kocha huyo aliigia kwenye mzozo na uongozi wa timu hiyo kufuatia kuanika hadharani suala la ukata lililokuwa liikabiri timu yake na hatimaye suala hilo likamalizwa kwa wachezaji kupatiwa haki zao.
Post a Comment