Mar 30, 2012

Posted by Dismas Ten Friday, March 30, 2012 No comments
Kikosi cha Villa Squad

Zikiwa zimesalia takriban raundi nne kabla ya kumalizika kwa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara Kocha Mkuu wa timu ya Villa Squared yenye maskani yake Kinondoni jijini Dar es Salaam Habib Kondo amesema ana uhakika kikosi chake hakitateremka daraja.

Aakizuangumza na Blog Hii mapema jana Kocha huyo anayetajwa kuwa na umri mdogo kuliko makocha wote wanaofundisha timu zinazoshiriki ligi hiyo alitanbaisha kuwa matokeo mazuri waliyoyapata katika michezo mitatu ya hivi karibu yamempa matumaini makubwa ya kusalia katika ligi hiyo msimu ujao huku pia akipiga mahesabu ya kupata pointi zingine katika michezo minne waliyobaki nayo.

"Kila mmoja ameona tumekuwa na matokeo mazuri katika michezo mitatu iliyopita, nina imani ya kupata pointi zingine kwenye michezo minne iliyosalia na kujihakikishia nafasi ya kubaki kwenye ligi msimu ujao kwa uwezo wa mungu nina uhakaikia timu yangu haitashuka daraja" alisema Kondo.

0 COMMENTS:

TAFUTA HAPA

UNGANA NASI

Delicious Digg Facebook Favorites More Stumbleupon Twitter