
Katika makabidhiano hayo yaliyofanyika jana jijini humo mkuu wa mkoa huo Eng.Evarist Ndikilo aliutaka uongozi wa klabu hiyo kuutumia vizuri msaada huo ili usaidie katika kuiepusha timu hiyo na hatari ya kutelemka daraja hatimaye jiji hilo likakosa uwakilishi katika michuano ya Ligi kuu.
"Ni juzi tu tumetoka kusikio malalamiko ya ukata mkubwa uliokuwepo klabuni hapa, tunawashukuru GGM kwa msaada wao lakini nawaomba mtumie vizuri msaada huu ili tusije tukajikuta bado tunaendelea kubaki kwenye hatari ya kutelemka daraja na hatimaye Mwanza ikabaki kucheza mashindano ya ngazi za chini" alisema Ndikilo.
Katika hatua nyingine kampuni hiyo pia imetoa kiasi kama hicho kwa ajili ya kuisaidia timu maarufu ya Pamba Sc inayoshiriki ligi daraja la kwanza ili iweze kujipanga na hatimaye kurejea tena katika ligi kuu .
Post a Comment