Shamte Ally wa Yanga akiruka juu kukwepa daruga la mlinzi wa Toto African.
Katibu Mipango wa klabu ya Toto African ya jijini Mwanza Hassan Kilaka amesema kufanya vibaya kwa timu hiyo hivi sasa katika michuano ya Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara kunatokana wadau wa soka jijini humo kuitelekeza timu hiyo.
Akizungumza na SLT kwa njia ya simu kutoka Mwanza mapema leo kiongozi huyo alitupa lawama kwa wadau hao kuwa wameacha mzigo wote wa kuindesha timu hiyo mikononi mwa uongozi alhali wakijua kuwa hauna uwezo wa kutosha.
"Hivi sasa timu hii ni kama imesuswa mikononi mwa viongozi hakuna mdau yoyote anayejitokeza kusaidia kwa jambo lolote katika kuhakikisha kuwa timu inafanya vizuri alisema" Kilaka.
Toto African ni moja ya timu zilizo katika hatari ya kushuka daraja endapo zitashindwa kufanaya jitihada za kweli za kujinasua kwani mpaka sasa iko kwenye nafasi ya 12 ikiwa imekusanya jumla ya poiti 13 baada ya kuteremka dimbani mara 15.

0 COMMENTS:
Post a Comment