Mar 30, 2012

Posted by Dismas Ten Friday, March 30, 2012 No comments
Kiungo wa timu ya Taifa ya Zanzibar, Abdulhareem Humud, anayekipiga nadi ya kikosi cha Azam FC, amesema timu yake inaweza kukosa ubingwa wa ligi kuu ya soka Tanzania Bara kwa Simba lakini siyo kwa mabingwa watetezi Yanga.

Akizungumza na Blog hii mapema leo, Humud aliyewahi kuichezea pia Mtibwa Sugar ya Turiani alisema kuwa ubora iliyonawo Simba hivi sasa hasa kwenye nafasi ya ushambuliaji unampa homa kubwa kuwa huenda timu hiyo ikafanikiwa kutwaa ubingwa wa ligi hiyo tofauti na Yanga mabayo imeonyesha kutokuwa sawa upande wa ushambuliaji katika siku za hivi karibuni.

"Unajua hivi sasa Simba wako vizuri sana kwenye ushambuliaji tofauti na Yanga nahisi tunawezxa kuukosa ubingwa kwa Simba lakini siyo Yanga" alisema Humud

katika hataua nyingine nyota huyo anayetajwa kuwa mmoja wa viungo weneye uwezo mkubwa nchini alisema kuwa hivi sasa amerejea kwenyen kiwango chake na na imani kocha wa timu ya taifa Jan Poulsen atamjumuisha kwenye kikosi hicho wakati wowote.

0 COMMENTS:

TAFUTA HAPA

UNGANA NASI

Delicious Digg Facebook Favorites More Stumbleupon Twitter