Nyota wa soka
Bongo, Jerry son Tegete, anayekipiga
kwenye kikosi cha mabingwa wa zamani wa
soka Tanzania Bara Yanga , amesema hana mpango wowote wa kuipa kisogo timu yake katika kipindi kijacho cha usajiri wa majira ya joto licha ya
kuvurunda msimu huu.
Akizungumza na
blog hii mapema leo Tegete
ametanaibaisha kuwa licha ya timu yake
kukosa Ubingwa wa Ligi ya Tanzania Bara msimu huu bado anataka kubaki kwenye kikosi hicho kwa kuwa
anaimani kubwa kuwa uongozi wa timu hiyo utafanya marekebisho
makubwa na kuifanya Yanga kuwa bora zaidi
msimu ujao.
“Ni wazi kuwa tumekosa ubingwa msimu huu, sina mawazo ya
kuondoka Yanga, nataka kubakia hapa, nina
imani msimu ujao tutakuwa na kikosi bora
zaidi kuliko msimu huu, hii ni kwa sababu
najua uongozi utafanya marekebisho makubwa ikiwa ni pamoja na usajiri wa
nguvu katika kuuimarisha timu” alisema
Tegete.
0 COMMENTS:
Post a Comment