Na Hemed Kisanda
Zikiwa zimesalia siku
chache kabla ya kupigwa kwa mchezo wa
watani wa jadi kwenye soka la
Bongo hapo Mei mwaka huu, uchunguzi
uliofanywa na blog hii
kutoka kwa wadau mbalimbli
wa soka
umeonyesha kuipigia upatu Yanga
kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 kwenye mcheo huo.
Wakizungumza kwa nyakati
tofauti kuhusu mechi hiyo inayotarajia kupigwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar,
mashabiki wengi mamepiga kura ya
kuipa ushindi Yanga kwa madai kuwa itaingia uwanjani kwa kukamia
ikiwa na lengo la kulinda heshima
yake hasa baada ya kuambulia patupu
kwenye michuano ya ligi kuu mwaka huu.
“Unajua ndugu yangu huu
ni msimu mbaya kwa Yanga kwa
kuwa haina lolote la kujivunia, naamini wataingia uwanjani kutka kurinda
heshima na kuwapa faraja mashabiki wao , binafsi nahisi wanweza kupaa ushindi
wa 2-1 dhidi ya watani zao” alisema
shabiki mmoja aliyejitambulisha
kwa jina la Saddam na kudai kuwa yeye ni shabiki wa kutupwa wa Ashanti United.
Kaika hatua nyingine
shabiki mmoja wa Simba ambaye
hakupenda kutajwa jina lake alisema kuwa ana
hofu timu yake itaingia uwanjani ikiwa
imejiamini kupia kias jambo amabalo linaweza kuifanya Simba ikapoteza mchezo
huo.
“Hakika timu yetu ni nzuri kwa sasa lakini
wasiwasi wangu ni kupoteza mchezo endapo
wachezaji wataingia uwanjani wakiwa wamejiamini kupita kiasi na kuidharau Yanga alisema shabiki huyo.
0 COMMENTS:
Post a Comment