Kiungo mahiri wa mabingwa wa soka msimu uliopita nchini, Yanga Haruna Niyonzima, amesema hana mpango wa kuondoka katika timu yake hiyo kwa wakati huu ikiwa ni kulinda heshima ya Rais wa nchi yake Paul Kagame.
Akizungumza na SLT mapema mchana huu kutoka kwenye kambi ya timu hiyo Wilayani Bagamoyo, Haruna ambaye pia ni nahodha wa timu ya taifa ya Rwanda (Amavubi) amesema kuwa hafikirii kuipa mkono wa kwaheri Yanga kwa kuwa kufanya hivyo atavunja makubaliano aliyofanya na Rais Kagame wakati wa usajiri wake kutoka APR.
"Unajua wakati natoka APR kuja Yanga nilitumia zaidi ya saa mbili kwenye ikulu ya Rwanda nikizungumza na Rais juu ya mimi kuicha timu yake kuja Yanga, kimsingi tulizungumza mengi lakini kikubwa alichoniambia muheshimiwa ni kuwa kama itatokea nimeshindwa kuendelea kuitumikia Yanga basi nimwambie na mara moja atanitumia ndege kunirudisha nyumbani kwenye kikosi cha APR" alisema HARUNA
Akiendelea zaidi haruna alisema kuwa awali aliwahi kujaribu kwenda kucheza katika nchi kadhaa ulaya kama Ufaransa Sweden na Uturuki lakini mara zote rais Kagame alikuwa akimrudisha kabla ya kumaliza majaribio yake ili aisaidie APR.
"MARA kadhaa nilijaribu kwenda Ulaya kucheza lakini alikuwa akinirudisha kabla sijamaliza majaribio kwa kuwa alitaka niendelee kuichezea APR hivyo hata kuja hapa aliniruhusu kwa shingo upande huku akinia maagizo hayo na kubwa zaidi likiwa ni kuwa hata yeye anaipenda YANGA" alimaliza Haruna
0 COMMENTS:
Post a Comment