Na Hemed Kisanda
Msemaji wa klabu ya Simba Ezekiel Kamwaga (Mr Livepool) ametamba kuwa licha ya shirikisho la soka nchini TFF kuusogeza mbele mchezo wa mwisho wa ligi kuu ya soka Tanzania Bara dhidi ya watani zao Yanga ana uhakika kikosi chake kitaibuka na ushindi mnono wa bao 3-0.
Akizungumza na SLT mchana huu kamwaga amesema kuwa tambo hizo zinatokana na ushindi wa idadi hiyo ya mabao iliyoupata timu yake kwenye za hivi karibuni katika ligi hiyo na ule wa kombe la shirikisho dhidi ya Al Ahly Shandy ya Sudan.
"Najua vijana wataendeleas rekodi yetu ulioyoiona katika mechi za hivi karibuni kwenye ligi na pia kwenye kombe la shirikisho kila timu tuliyokutana nayo imekula bao 3 na hata watani zetu kipigo chao kitakuwa ni hicho"alisema Kamwaga
0 COMMENTS:
Post a Comment