Siku chache baada ya kupokea kipigo cha bao 5-0 kutoka kwa watani zao Simba katika mchezo wa mwisho wa ligi kuu Tanzania bara uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa jumapili iliyopita wadau na mashabiki wa Yanga jijini mwanza wameibuka na kumtaka mwenyekiti wa timu hiyo Lloyd Nchunga kujiuzuru.
wakizungumza na blog hii mapema leo mashabiki hao wamesema kuwa hakuna utawala mbovu uiliwahi kutokea ndanai ya klabu yao kama huu uiliopo sasa hivyo mwenyekiti huyo ameshindwa kuiongoza klabu hiyo.
"Tunamtaka mwenyekiti ajiuzuru kwani inatuuma sana kufungwa bao 5 na watani zetu, hakika huu ni uongozi mbovu kuwahi kutokea katika timu yetu , tunamkumbuka sana mwenyekiti alieyepia (Madega) licha ya kuwa alikuwa na mapungufu yake lakini klabu haikuyumba na kugawinyika kama ilivyo sasa" walisema Wadau hao.
0 COMMENTS:
Post a Comment