Jun 6, 2012

Posted by Dismas Ten Wednesday, June 06, 2012 1 comment
                                                    BONIFACE WAMBURA
Kiingilio cha mchezo wa  pili wa  kusaka  tiketi ya kushiriki michuano  ya  kombe la  dunia 2014  inayotarajiwa  kuchezwa  nchini  Brazil baina ya  timu ya soka  ya  Taifa,, Kilimanjaro Taifa  Stars na  Gambia   kimetajwa.

Akizungumza na  blog hii  muda mfupi uliopita, msemaji wa  shirikisho la kandanda  nchini, Boniface Wambura,  amesema kuwa TFF imepanga  kiingilio cha kawaida   kulingana  na mazingira halisi ya maisha ya wapenda soka  hapa nchini.

"Tumeamua kuweka kiingilio cha kawaida ili kuwapa nafasi Watanzinia kujitokeza kwa wingi kuishangilia timu yao huku pia tukiangalia halisi ya maisha  kwa  wapenda soka  wote hapa nchini". alisema Wambura na kuongeza  kuwa  huu ni mchezo ambao Stars  inahitaji sapoti zaidi kutoka kwa  mashabiki wa  mchezo huo na tunaimani kubwa  kuwa  kwa  kiingilio hiki kidogo  watu watajikeza kwa wingi kuishangilia  timu yao.

Akiendelea zaidi Wambura alisema   kuwa  shirikisho hilo limejipanga  kuhakikisha  Stars inaibuka na ushindi katika mchezo huo  na kuweka hai matuamini ya kufuzu kwa fainali  hizo za  Brazil.

 Mpangilio wa  viingilio  utakuwa  kama ifuatavyo:

Kwa  viti vya  kijani na blue  Kiingilio  kitakuwa  Shilingi  3000.
Kwa viti vya rangi ya machungwa  kiingilio kitakuwa  Shilingi 5,000.
Kwa upande wa majukwaa makuu  V.I.P C  itakuwa shilingi   10,000
Kwa upande wa  V.I.P.   B kingilio kitakuwa  shilingi     20,000 na  mwisho VIP A  kiingilio kitakuwa  shilingi  30,000.

Katika  hatua nyingine  Wambura alitanabaisha kuwa  maandalizi ya mchezo huo yanakwenda  vizuri ikiwa  ni pamoja na  kufahamikwa  kuwa  waamuzi wa mtanange huo kuwa watatoka nchini Zimbabwe. 

1 COMMENTS:

Anonymous said...

MUHIMU TIKITI ZIANZE KUUZWA KESHO

TAFUTA HAPA

UNGANA NASI

Delicious Digg Facebook Favorites More Stumbleupon Twitter