KOCHA mkuu wa timu ya soka ya Taifa ya Tanzania ( Kilimanjaro taifa stars), Kim Poulsen, (pichani) anatarajia kukutana uso kwa uso na kocha wa timu ya Taifa ya Gambia, Lucio Mancini, jumamosi hii.
Akizungumza na blog hii mapema leo Poulsen alisema kuwa nataraji kukutana na kocha huyo katika kikao maalum kitakachofanyika siku moja kabla ya mchezo ili kuweza kujadiri mambo kadhaa kuelekea mchezo huo.
"Nataka kukutana na Manchini jumamosi, hatufamiani sana lakini nahisi kuna mambo ya kuzungumza na nimependekeza iwe saa nne asubuhi ili baada ya kikao tuweze kuendelea na ratiba zingine kuelekea mchezo wetu mwishoni mwa wiki". alisema Pousen
katika hatua nyingine kocha huyo raia wa Denmark ametamba kuwa kikosi chake kiko imara kuipa kicha kiali Gambia na kijiwekea mzungira mazuri kueleka huko nhcini Brazil.
"sina wasiwasi kikosi changu kiko imara na tunendelea na mazoezi kama unavyoona asubuhi tupo hapa karume na jioni ya leo tutakuwa kwenye uwanja wa taifa tukijiweka sawa tayari kwa kutoa dozi kwa wapinazani wetu". alimaliza Poulsen. huku akisifia uwepo wa nyota wa timu ya TP mazembe, Mbwana Samatta.
0 COMMENTS:
Post a Comment