Jun 7, 2012

Posted by Dismas Ten Thursday, June 07, 2012 No comments
 Kamapuni ya  vinywaji baridi  ya  Coca Cola  inayodhamini  michuano maarufu  ya  vijana kwa upande wa  soka  ijulikanayo kama  Copa Coca Cola  imeahidi  kuwatunza na kuwaendelea  nyota  watakaopatikana katika michauano ya mwaka huu.

Akizungumza  na blog hii  muda mfupi mara baada ya kumalizika  kwa  upangaji wa droo ya  michuano hiyo kwa mwaka huu,  mwakilishi wa  mdhamini   kutoka kampuni hiyo  Bwana  Evance Mdelwa, amesema   kampuni yake  imejipanga  kuhakikisha kuwa nyota watakao patikana katika michuano hii  wanatunzwa na kuendelezwa  vizuri tofauti na ilivyokuwa katika  misimu kadhaa iliyopita.

"Ndiyo, kama wadhamini  tumegundua kuwa  kuna  haja ya  kuwalinda, kuwatunza  na kuwaendeleza  nyota wa michuno ya mwaka huu  ili kuleta maana halisi ya  michuno hii  na hatimaye taifa liweze kupata wachezaji wa kweli wenye maadili yote watakoweza kuleta manufaa  kwa siku za usoni"  alisema Mdelwa.

Akiendelea zaidi Mdelwa  ameweka wazi  nia ya  kampuni hiyo  kuboresha zaidi michuano hiyo  na  kuifanya  kuwa nguzo  kubwa ya  kusaka vipaji kwa soka la  Tanzania.

katika  hafla hiyo ya upangaji wa Droo  iliyofanyika  makao makuu ya  shirikisho la soka nchini TFF, michuano hiyo imepangwa kupigwa katika viwanja vinne tofauti  kwa  michezo ya  asubuhi na jioni,  viwanja  vilivyopagwa kutumika katika  kinyang'anyiro hicho ni Karume, Nyumbu Kibaha, Tamko Kibaha, na Kawe jiijini Dar.


  

 

0 COMMENTS:

TAFUTA HAPA

UNGANA NASI

Delicious Digg Facebook Favorites More Stumbleupon Twitter