Kikosi kamili cha Timu ya soka ya Taifa ya Gambia kinataraji kutua leo usiku tayari kabisa kuivaa Taifa star katika mchezo wa pili wa kusaka tiketi ya kushiriki michuano ya Kombe la dunia 2014 inayotajiwa kutimua vumbi huko nchini Brazil.
Akizungumza na blog hii muda mfupi uliopita msemaji wa shirikisho la soka nchini TFF, Boniface Wambura amesema kuwa Timu hiyo itawasiri kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jk Nyerere majira ya saa 3:30 usiku ikiwa na msafara wa watu 32, kati yao 22 wakiwa ni wachezaji na waliobaki ni viongozi tayari kwa kuikabiri Stars hapoa siku ya jumapili.
"Ndiyo Gambia ilikuwa iwasiri jana lakini ilishindwa baada ya kuchelewa kubadili ndege ilipokuwa jijini Dakar Senegal hivyo itawasili leo muda huo ikiwa na kikosi kamili kwa mujibu wa viongozi walioambatana na timu hiyo kutoka shirikisho la mpira huko Gambia". alisema Wambura
Akiendelea zaidi msemaji huyo alitanabaisha kuwa timu hiyo itaweka kambi katika Hotel ya Sawaya, na itakuwa na program ya mazoezi kuanzia kesho asubuhi kwenye uwanja wa Karume na baadae uwanja wa Uhuru siku ya Jumamosi.
Katika hatua nyingine Wambura alisema kuwa tiketi za mtanange huo sitaanza kuuzwa siku ya jumamosi asubuhi katika vituo vyote ambavyo shirikisho hilo limekuwa likivitumia kwenye michezo iliyopita.

0 COMMENTS:
Post a Comment