Jun 7, 2012

Posted by Dismas Ten Thursday, June 07, 2012 No comments
 Nyota  wa  kikosi cha  Timu ya Taifa ya Tanzania , Nurdin Bakari na Thomas Ulimwengu wamepona majeraha yaliyokuwa  yanawasubua  na watakuwa tayari kuingia uwanjani  jumapili hii kwenye mchezo  dhidi  ya Gambia.

Akizungumza na Blog  hii mapema leo , msemaji wa  TFF, Boniface Wambura  amesema kuwa, asubuhi ya leo nyota hao walikuwa wakifanya mazoezi mepesi  ili kujiweka  sawa tayari kwa mazoezi kamili hapo kesho na  jumamosi pia.

Ni kweli  wako safi kwa mujibu wa taarifa ya daktari ndiyo mana aleo umeona wameanza mazoezi mepesi, lakini hakuna shaka yoyote juu yao na nina uhakika  mwalimu atawatumia   katika mchezo wa jumapilia  dhidi ya Gmabia  alisema Wambura.

Katika hatua nyingine msemaji huyo aliarifu kuwa  hali ya kiungo Haruna Moshi Boban bado haijwa  sawa na  huenda akakosa  pia  mchezo huu  wa jumapilia  ingawa  daktari wa timu bado hasibitisha hilo.
 

0 COMMENTS:

TAFUTA HAPA

UNGANA NASI

Delicious Digg Facebook Favorites More Stumbleupon Twitter