Wagombea 26 wamepitishwa katika kinyang’anyiro cha
kugombea nafasi za uongozi katika  klabu
ya Yanga  kufuatia  kujiuzuru kwa 
Mwenyekiti  Lloyd Nchunga.
Akizunguma  na Blog 
Hii muda  mfupi  uliopita 
msemaji wa  klabu hiyo yenye  makao yake makuu mtaa wa Jangwani  jijini Dar es Salaam Louis Sendeu   amesema kuwa, taarifa  ya 
pingamizi kwa mgombea yoyote 
inatakiwa  kutolewa  kuanzi tarehe 14 na 18 huku siku hiyo ya  mwisho 
ikiwa  pia ndiyo  siku ambayo wagombea hao 26 watafanyiwa  usaili 
tayari kwa uchaguzi.
“Wamepitishwa
waombea  26 hivyo  tusubiri 
kuona  kama  kutakuwa na pingamizi lolote na kama  kutakuwa 
hakuna  basi  moja kwa moja tutakuwa  tusubiri 
kuona  nani ataibuka mshindi  kwenye 
uchaguzi  unaokuja”  alisema 
Sendeu.
 

















 
 
 
0 COMMENTS:
Post a Comment