Jun 11, 2012

Posted by Dismas Ten Monday, June 11, 2012 No comments

 BABA mzazi wa mshambuliaji wa Yanga, Jerry Tegete,Mzee  John Tegete amefurahishwa  na  uamuzi wa mlinzi wa  klabu ya  Simba, Kelvin Yondani kujiunga  na wapinzani wao Yanga.

Akizungumza na Blog hii mapema  leo Mzee Tegete ambaye pia  ni kiongozi  wa timu ya Mwanza Veterani  alisema kuwa maamuzi ya Yondani kwenda Yanga ni sahihi, kutoka  na  tuhuma  nyingi alizokuwa  akibebeshwa  hapa na pia kwa ajili ya maisha yake ya baadae.

 “Yondan amejiunga Yanga, ni bora  kwa maslahi ya maisha yake ya baadae na pia hataua hiyo itamuepusha na lawama  alizokuwa akitupiwa  mara kwa mara pindi timu hizo zinapokutana na Simba kupata matokeo mabaya” alisema Mzee Tegete.

Katika  hatua  nyingine Mzee huyo ambaye ni baba  mzazi wa mshambuliaji nyota wa Yanga Jerry Tegete alitamba kuwa yeye na wazee wengine jijini Mwanza ndiyo walimshawishi nyota huyo kutua jangwani.
“Sisi ndio tuliyempeleka Kelvin Yanga, ni vizuri Simba  wakakubariana na mawazo yake kwani huu ni  mpira na siyo vita, namshangaa  Rage kuwarushia watu maneno makali wakati mchezaji huyo hakua na  mkataba na klabu yao” aliamaliza Mzee huyo. 

Yondani amesaini mkataba wa miaka miwili ya kuichezea Yanga kwa kitita cha shilingi milioni 30  na kuibua utata mkubwa baina ya timu hizo mbili.

0 COMMENTS:

TAFUTA HAPA

UNGANA NASI

Delicious Digg Facebook Favorites More Stumbleupon Twitter