MSHAMBULIAJI
wa Coastal Union ya Tanga , Ben Mwalala kuikacha timu hiyo kuelekea falme za
kiarabu kucheza soka ya kulipwa.
Akizungumza na Blog hii
muda mfupi uliopita Mwalala
ametanabaisha kuwa atatimkia urabuni kujiunga
na klabu ya klabu ya Al- Teliya mara baada ya kumalizika kwa michuano ya
Kombe la Kagame.
“Ni
meambia kuwa sitakuwa katika kikosi cha Coastal Union msimu ujao hivyo nimeona ni bora kwenda kusaka maisha mengine huko Uarabuni” alisema
Mwalala.
Akiendelea
zaidi Mwalala aliyewahi kuitumia Yanga ya
jijini Dar, aliarifu kuwa ni kawaida kwa mchezaji kutokujumuishwa kwenye kikosi kutokana na sababu mbalimbali ndiyo maana
haja lalamika na amepanga kuelekeza nguvu zake
huko Uarabuni .
“ Kabla ya kuja Coastal nilikuwa
nacheza soka kwenye klabu hiyo,
ndiyo maana imekuwa rahisi kwangu kurudi kwa mara nyingine na
ninatarajia kuondoka hapa mara baada ya
kumalizika michuano ijayo ya kombe la Kagame,” alisema Mwalala.
Mwalala ni
miongoni mwa wachezaji tisa waliotemwa na Coastal Union katika msimu ujao wa ligi kuu ya Bara sambamba na Ali
Ahamed ‘Shiboli’.
0 COMMENTS:
Post a Comment