Jun 9, 2012

Posted by Dismas Ten Saturday, June 09, 2012 No comments
 Shirikisho la soka  nchini TFF liko kwenye mchakato wa kusaka kocha mpya wa timu ya  vijana  atakayerithi  mikoba ya kocha wa zamani Kim Poulsen ambaye sasa anaifundisha timu ya  wa kubwa Taifa Stars.

Afisa wa habari wa shirikisho hilo  Boniface Wambura  ameiambia  Blog  hii  kuwa mchakato huo  uko kwenye hatua nzuri kwani mpaka sasa  makocha  wengi kutoka mataifa mbalimbali duniani kote  wametuma mambi kutaka kazi hiyo.

"Mchakato unaenda vizuri kwani mpaka sasa  tumepokea maombi ya makocha wengi  kutoka sehemu mbalimbali wakitaka  kufundisha timu yetu ya vijana" alisema  Wambura

Akiendelea zaidi msemaji huyo aliarifu  kuwa  mchakato huo unamuhusisha  pia kocha mkuu  wa Taifa Star  Poulsen kwa kuwa  falsafa  ya shirikisho hilo  ni kuhakikisha kuwa  kama kocha mkuu wa timu ya wakubwa anatoka  Denmark  basi na watimu ya vijana lazima atoke katika nchi hiyo.

"Falsafa  yetu ni  kuona makocha wa timu zote wanatoka  sehemu moja   ndiyo mana  tunamshirikisha mwalimu  Poulsen katika  mchakato huu  ili kupata mtu sahihi  ambaye  wanaweza kushirikiana  kutengeneza  timu nzuri pande zote"  alimaliza  Wambura 


0 COMMENTS:

TAFUTA HAPA

UNGANA NASI

Delicious Digg Facebook Favorites More Stumbleupon Twitter