Tiketi za pambano na kuwania kufuzwa kwa michuano ya kombe la dunia 2014 katika ya Taifa Stars na timu ya taifa ya Gambia zitaanza kuzwa kesho katika vituo mbalimbali.
Akizungumza na blog hii muda mfupi uliopita msemaji wa shirikisho la soka Tanzania, Boniface Wambura amesema kuwa tiketi hizo zitauzwa katika maeneo ya Stears Posta, Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa,Uwanja wa Taifa na maeneo ya Soko Kuu la Kariakoo.
"Tiketi zitaanza kuuzwa kesho majira ya saa mbili kwenye vituo hivyo, kwa kiingilio ambacho tulishatangaza hapoa awali, hivyo tunawaomba watanzania kujitokeza kwa wingi kupata tiketi kwa ajili ya kwenda kuipa sapoti timu yao" alisema Wambura
Akiendelea zaidi msemaji huyo aliarifu kuwa tiketi hizo zitapatikana pia Uwanja wa Taifa siku ya mchezo kuanzia majira ya saa 5 mara baada ya kufungwa kwa vituo vilivyo nje na uwanja huo.
Katika hatua nyingine Wambura amesema kuwa Nahodha wa timu ya Twiga Stars Sofia Mwasikili ameshindwa kuwasiri jana kama alivyotarajiwa baada ya kuchelewa ndege jijini Istambul.
"Sofia ameshindwa kuwasili jana usiku kama tulivyo watangaziam kutokana na kuchelewa ndege hivyo amepangiwa ratiba nyingine na anatarajiwa kuwasili hapa nchini siku ya jumapili" alisema Waambura.

0 COMMENTS:
Post a Comment