Dec 31, 2009

Posted by Dismas Ten in | Thursday, December 31, 2009 No comments
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania MH.Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa kifo cha MH.Rashird Mfaume Kawawa aliyewahi kuwa waziri mkuu wa Tanzania wakati wa uhai wake kilichotokea leo asubuhi majira ya saa tatu na dakika 20 asubuhi ni pigo kubwa kwa taifa hili kutokana na mchango mkubwa aliokuwa akiutoa.
Katika hatua nyingine MH Kikwete amesema kuwa Serikali itasimamamia shughuli nzima ya mazishi ya Mzee Kawawa kama mbavyo imekuwa ikisimamia matibabu yake na pia ametangaza kuwa kwa heshima ya mzee Kawawa Bendera ya Taifa itapepea nusu mlingoti kwa muda wa siku saba kuanzia leo

Dec 28, 2009

Posted by Dismas Ten in | Monday, December 28, 2009 No comments
Amr Zaki may have declared himself fit for the 2010 Africa Cup of Nations, but it appears the Egyptian technical team have no plans to use him in Ghana.
The Zamalek striker, once the toast of Europe as he was banging in the goals for Wigan Athletic in the English Premiership in the first half of last season, has struggled with a hamstring injury of late.
But he declared himself fit over the weekend and ready to help The Pharaohs to a third-successive African continental title, but he has allegedly been told to forget about it by national team coach Hassan Shehata.
Shehata has had his problems up front, but was able to include Zaki's Zamalek teammate Mido in his preliminary squad for the tournament.
The other forwards in the squad are Emad Meteb (Al Ahly), Ahmed Raouf (ENPPI), Al-Sayed Hamdi (Petrojet), Geddo (Ittihad), Mohamed Zidan (Dortmund, Germany), with the final 23-man selection to be named before the deadline of December 31.
Posted by Dismas Ten in | Monday, December 28, 2009 No comments
Papa Benedict alitoa ujumbe wake wa Krismasi siku ya Ijuma, saa chache baada ya kuangushwa chini na mwanamke aliyemvamia wakati wa misa ya mkesha ilipoanza katika kanisa la St Peter's Basilica.
Maafisa wa Vatican wameleza kwamba, Papa mwenye umri wa miaka 82 hakujeruhiwa na ratiba yake ya Krismasi iliendelea kama ilivyopangwa. Akizungumza kwa lugha 65 tofauti kutoka baraza kuu ya kanisa, kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki alisoma dua kwajili ya amani na furaha wakati huu wa sikukuu.
Katika ujumbe wake Papa Benedict, alizungumzia athari za mzozo wa fedha duniani, mizozo huko eneo Takatifu na Afrika, na maafa yanayowapata aliyewataja kundi dogo la wakristo huko Iraq. Alisema mara kwa mara wa kristo wa Irak wanakabiliwa na ghasia na kunyanyaswa.
Kiongozi huyo alitoa ujumbe wake kwa wakati ulopangwa, saa chache baada ya kuvamiwa na mwanamke mwenye umri wa miaka 25. Maafisa wa usalama wa Vatican wanasema yeye ndiye mwanamke yule yule aliyevuka vizuizi na kumkaribia Papa wakati wa misa ya Krismasi mwaka jana.
Hakuna sababu zilizotolewa za mwanamke huyo za kufanya shambulio, lakini maafisa wanasema ni mtu mwenye matatizo ya kiakili. Kardinali wa Kifaransa Roger Etchegaray alijeruhiwa wakati wa tukio hilo.

Dec 23, 2009

Posted by Dismas Ten in | Wednesday, December 23, 2009 No comments

Star wa Hip Hop nchini Marekani John David Jackson a.k.a Fabolous ameamsha mjadala mkubwa miongoni mwa mashabiki wake baada kutamka kuwa ana shauku kubwa ya kukaa meza moja na kiongozi mkuu wa kundi la magaidi la El Qaida, Osama bin Laden.

Nyota huyo wa muziki aliwahi kutamba na albam ta Street dream aliyasema hayo muda fupi baada ya kukutana na mtoto wa gaidi huyo Omar Osama bin laden kwenye duka moja la mavazi Jijini Rabat nchini Morocco.

Nasikia habari kutoka kwa watu mbalimbali kuwa baba yako ni tajiri mkubwa licha ya kuonekana ni adui wa kila mtu nina shauku kubwa ya kukuta nae siku moja ili anipe mbinu za kuwa tajiri kama yeye, Fabolous alimwambia Omar huku waliwa wameshikana mikono ndani ya duka hilo.

Hata hivyo Omar hakujibu chochote kuhusu hilo zaidi ya kucheka na kumwambia Fab kuwa hata yeye ni shabiki wake mkubwa.
Posted by Dismas Ten in | Wednesday, December 23, 2009 No comments

Kijana mmoja maarufu kwa maonyesho ya maigizo nchini Canada, Sunday Kewel ameoteza maisha baada ya kamba aliyokuwa anaitumia kuigiza kaka mtu alijinyonga kumnyoga kweli na kuaga dunia

Ishu hiyo ilitokea kwenye onyesho lililofanyika wiki iliyopita kwenye ukumbi wa Otawa Theater uliopo jiini Otawa

Imeelezwa kuwa licha ya Sunday luonyeshs kali ya kutatapa lakini mashabiki waliokuwa wakishuudia waliendelea kumshangilia kwa kumpigia makofi na kusema anapatia sana kuigiza kama mtu aliyejinyonga bila kujua kuwa Sunday yuko kwenye hatua za kukata roho kutokana na kamba aliyokuwa akitumia kumnyonga kikweli

Mara baada ya kuona kijana Sunday ametulia tuli mashabaiki hao wa maigizo walinyamaza na kuanza kutahari kutaka kujua nini kinaendelea na ndipo msaidizi wa kijana huyo alipokwenda kumngusa na kutambua kuwa ameshakufa.

Baada ya kuataarifiawa hilo mashabiki hao walianza kupiga mayowe ya kumlilia Sunday na muda mfupi baadae polisi walifika na kutuliza taharuki hiyo na kuuchukua mwili wa marehemu.

Dec 10, 2009

Posted by Dismas Ten in | Thursday, December 10, 2009 No comments

Mapigano mapya yamezuka katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu jana Jumanne, na kuuwa watu wane na kuwajeruhi watu wapatao 20 wengine.

Mashahidi wanasema majeruhi wengi walitokea katika eneo la soko la Bakara, kaskazini mwa wilaya ya Hawl Wadaag huko Mogadishu. Mapigano yanaonekana kuwahusisha waasi na majeshi ya serikali ambayo yamekuwa yanapigana kuudhibiti mji mkuu.

Serikali dhaifu ya Somalia, inazidi kupata shinikizo la kuchukua hatua kali dhidi ya wanamgambo wa ki-Islam hasa al-Shabab. Kundi hilo la uaso linaaminika kuwa na ushirikiano na wanamgambo wa al-Qaida.
Posted by Dismas Ten in | Thursday, December 10, 2009 No comments


Kenya imekuwa ni nchi ya pili barani Afrika baada ya Afrika Kusini kuzindua mfumo wa teknolojia ya utangazaji wa televisheni kwa kutumia mitambo ya digital kama ilivyo kwenye mataifa yaliyoendelea .

Hii ina maana kwamba kuanzia mwezi Juni mwakani vituo vyote vya utangazaji wa televisheni nchini Kenya vitatumia mfumo huo mpya wa utangazaji baada ya kuondolewa kwa mfumo wa sasa wa analog.

Rais wa Kenya Mwai Kibaki alizindua mfumo huo na kusema kuwa uzinduzi wa mfumo huo ni muhimu sana kwasababu utaiweka nchi ya Kenya katika upeo mpya wa utangazaji.

Afrika Kusini ilikuwa nchi ya kwanza kupata mitambo hiyo barani Afrika. Wataalam na waandishi wa utangazaji wamesema Kenya imelazimika kuzindua mfumo huo ili kutekeleza agizo la shirika la mawasiliano duniani (ITU) yanayotaka mataifa yote duniani kuzingatia mfumo huo wa utangazaji ifikapo 2015.

Dec 2, 2009

Posted by Dismas Ten in | Wednesday, December 02, 2009 No comments

MWANAMUZIKI nyota wa miondoko ya pop na kipenzi cha akinadada kutoka pande za Marekani, Justin Timberlake a.k.a Handsome Boy, amewakata ngebe ‘masister du’ kibao duniani kote waliokuwa wakipigana vikumbo kuwania penzi lake baada ya kutoa kauli kuwa, hana wazo wala mpango wa kuoa kwa kwa sasa kutokana na kukabiliwa na majukumu mengi ya kufanya.

Kwa mujibu wa Jarida moja maarufu la kidaku nchini humo lijulikanalo kama Ok Magazine ambalo ndilo lilichapisha taarifa hiyo, linadai kuwa, sababu nyingine inayofanya handsome Boy huyo afute wazo la kuoa, ni kuiona ndoa kama kitanzi na aliwataka wale wote waliokuwa na matumaini ya kuolewa naye wasihangaike tena.

Hata hivyo, kauli ya Timberlake imepokelewa kwa mitazomo tofauti na wanyange waliokuwa wanawania kula bata na mwanamuziki huyo, ambapo baadhi yao walionekana kumuonea huruma mpenzi wake wa sasa wa nyota huyo, mwanadada Jessica Biel ambaye kwa upande wake ameonesha nia ya kumsubiri ajipange zaidi ili waweze kutimiza ahadi yao ya kuwa mke na mume siku za usoni.
Posted by Dismas Ten in | Wednesday, December 02, 2009 No comments

Katika hali ya kushangaza, mapema wiki hii Mwanamitindo mahiri nchini Ureno, Nereida Gallardo amewaambia waandishi wa habari kuwa, hatasahau kamwe maishani mwake siku ambayo alipata nafasi ya kujirusha na msukuma kandanda maarufu wa nchi hiyo Christiano Ronaldo ambaye kwa sasa anasukuma gozi kunako klabu ya Real Madrid ya Uhipania,

Habari zilizopatikana kwenye mtandao mmoja nchini humo zinasema kuwa, licha ya kutemwa katika mazingira ya ajabu na msukuma kandanda huyo, Nereida bado hana kinyongo naye na aliongeza kwamba, daima atamkumbuka na kama ikitokea atamuita tena kwa ajili ya mapenzi atafanya hivyo haraka bila kujali yuko upande gani wa dunia.

‘Siku hiyo baada ya kumalizika kwa zoezi la kupeana mapenzi moto moto, nililazimika kuwaomba wamiliki wa hoteli tuliyokuwa tumelala ili wakubali kuniuzia vitu vyote tulivyotumia ikiwa ni pamoja na mashuka na taulo ambazo mpaka leo hii nimevihifadhi vizuri kwenye moja ya makati yangu nyumbani na vitabaki kama kumbukumbu yangu muhimu.

Posted by Dismas Ten in | Wednesday, December 02, 2009 No comments

Rais wa Marekani Barack Obama anapeleka wanajeshi elfu thelathini zaidi wa Marekani nchini Afghanistan ifikapo kipindi cha majira ya joto mwaka 2010, na anapanga kuanza kuwaondoa mwaka unaofuatia. Rais alielezea mkakati wake wa kushinda vita nchini Afghanistan.

Baada ya miezi kadhaa ya kutafakari, Rais Obama ametangaza mpango wake wa kupeleka wanajeshi wa ziada nchini Afghanistan. Aliuzindua mkakati wake mbele ya wanajeshi kwenye kituo cha mafunzo ya kijeshi cha West Point huko New York, Jumanne jioni huku taifa likiangalia kwenye televisheni.

Wanajeshi wa ziada wataungana na wanajeshi wa Marekani wapatao 68,000 ambao tayari wapo Afghanistan, na maelfu ya wanajeshi wa ushirika.
Rais alizungumza huku uungaji mkono wa wamarekani ukizidi kupungua kuhusu vita. Utafiti mpya wa kituo cha Gallup unaonyesha asilimia 35 pekee ya wa-Marekani wanakubaliana na mkakati wa bwana Obama juu ya vita hivyo na asilimia 55 hawakubaliani naye.

Huko West Point, bwana Obama alisema Afghanistan haijapotea, lakini imekuwa ikirudi nyuma kwa miaka kadhaa. Alisema Al-Qaida inapanga vitendo vipya vya kigaidi kutoka hifadhi zake salama katika mpaka wa Afghanistan na Pakistan, kwa msaada wa Taliban.

Dec 1, 2009

Posted by Dismas Ten in | Tuesday, December 01, 2009 No comments

DADA KAMWAMBUKIZA BINTI YANGU UKIMWI PART 1.

MWANDISHI KULWA MWAIBALE

“Nilipokuwa mdogo naishi na wazazi wangu, sikufikiria kama katika maisha yangu ningeweza kukumbana na mikosi kama iliyonikuta na kunifanya nipoteze furaha ya kuishi na kutamani kufa kuliko kuendelea kuishi kwenye dunia hii iliyojaa mateso, simanzi na dhiki za kila aina.
Hata hivyo, ninapomwangalia binti yangu Mary ambaye kaambukizwa ugonjwa wa ukimwi ambao hauna tiba, namuomba Mwenyezi Mungu anipe uzima ili atakapotangulia mbele za haki nimzike kuliko kutangulia mimi na kumuacha akiteseka hapa duniani.
Jambo hilo nimekuwa nikimuomba sana mola wangu kwasababu naelewa nikifa na kumuacha Mary anayeugua maradhi hayo yasiyo na tiba, atateseka sana na kwa jinsi ninavyoona baadhi ya watu wasio na huruma watamnyanyapaa sana binti yangu.
Nasema hivyo kwasababu nimeshuhudia baadhi ya wagonjwa wa Ukimwi wakifanyiwa hivyo tena wengine na baadhi ya ndugu zao wa karibu au wa damu, hilo linaniumiza sana!
Mimi ni mkazi wa mjini Arusha ambaye kwasasa nina umri wa miaka 39.Nilioa mwaka 1993 ambapo nilijaliwa kupata watoto wawili ambao ni Mary aliyeambukizwa Ukimwi na dada yangu na mdogo wake Michael.
Baada ya kufunga ndoa na mke wangu ambaye tumetengana, maisha yalikwenda vizuri sana na upendo ulitawala katika nyumba yetu na kuwavutia watu wengi wakiwemo wazazi na ndugu zetu.
Sikuwahi kufikiria kama ingekuja kutokea siku moja tungetengana na mke wangu kipenzi, niliyempenda kuliko wanawake wote chini ya jua lakini mambo yalikwenda kinyume kwani tumetengana na mama watoto wangu na hivi sasa kila mmoja anaishi kivyake.

Kwanini bwana Mjema aliachana na mke wake kipenzi? Na nini chanzo cha bintiye Mary kuambikizwa Ukimwi na shangazi yake? Usikose kufuatilia mkasa huu wa kusisimua
Kupia blog hii
Posted by Dismas Ten in | Tuesday, December 01, 2009 No comments

Leo ni siku ya Ukimwi Duniani. Shirika la Afya Ulimwenguni limetoa takwimu zinaonyesha maambukizi ya ugonjwa ukimwi yamepungua kwa asilia mia 17 kote ulimwenguni.

Hata hivyo bado maambukizi katika nchi za kusini mwa jangwa la Sahara yako juu. Na huku nchi nyingi za Afrika. Ripoti ya Umoja wa Mataifa inasema watu milioni 33.4 wanaishi na virusi vya ukimwi kote duniani, kutoka milioni 33 mwaka 2007. Lakini la kutia moyo ni kwamba watu wengi wanaishi kwa muda mrefu kwa sababu ya uwezo wa kupata dawa za kupunguza maambukizi, zinazojulikana kama ARVS. Munira Muhammad alizungumza na Bruno Ghumpi, kaimu mkurugenzi mtendaji wa shirika la kiraia la kupambana na ukimwi, nchini Tanzania, WAMATA. Kwanza anaelezea changamoto wanazokabiliana nazo.
Posted by Dismas Ten in | Tuesday, December 01, 2009 No comments

Rwanda na Ufaransa jana Jumapili zimekubaliana kurudisha uhusiano wa kidiplomasia, miaka mitatu baada ya Rwanda kuvunja uhusiano.

Makubaliano hayo yalitangazwa na nchi zote. Rwanda ilivunja uhusiano na Ufaransa Novemba mwaka 2006, baada ya jaji mmoja wa uchunguzi wa Ufaransa kumshutumu Rais wa Rwanda Paul Kagame kuamuru mauaji ya mwaka 1994 ya mrithi wake, Juvenal Habyarimana. Ndege ya bwana Habyarimana ilitunguliwa huko Rwanda.

Tukio hilo lilionekana kuchochea mauaji ya halaiki ya Rwanda ambapo waasi wa kihutu waliwauwa watu wapatao laki nane. Katika maendeleo tofauti Rwanda imekubaliwa kujiunga na Jumuia ya Madola. Ni nchi ya 54 kujiunga na kundi hilo ambalo wanachama wengi ni makoloni ya zamani ya Uingereza.
Posted by Dismas Ten in | Tuesday, December 01, 2009 No comments

Maafisa barani Afrika wamekamata zaidi ya kilo elfu moja ya pembe haramu za ndovu, na kufanya ukamataji kadhaa katika uchunguzi wa mataifa mbali mbali juu ya uwindaji haramu na magendo.

Shirika la kimataifa la polisi-Interpol, lilisema jana Jumatatu uchunguzi uliwahusisha maafisa kutoka nchi sita za Kenya, Burundi, Ethiopia, Rwanda,Tanzania, na Uganda. Shirika hilo lilisema ukamataji huo wa pembe za ndovu ni mkubwa kuwahi kutokea.

Interpol ilisema maafisa katika nchi zote sita walifanya ukaguzi na kuvamia maduka na masoko. Maafisa pia walipekua magari katika vituo vya ukaguzi mipakani. Kwa kuongezea biashara haramu ya pembe za ndovu, Interpol ilisema uchunguzi huo uligundua ngozi za chui, na silaha.
Posted by Dismas Ten in | Tuesday, December 01, 2009 No comments

Mwanamuziki mahiri wa Pop pande za Marekani mwanadada Nivea ,ametoa taarifa kupia mtandao wa Twitter kuwa yeye na mpenzi wake Lil Wayne wanasubiri kwa hamu ujio wa mtoto wao anetarajiwa kuzaliwa hivi karibuni

Katika taarifa yake hiyo mwanadada huyo mwenye sura ya kuita alisema wiki iliyopita huko Miami walifanya sherehe kubwa iliyoandaliwa na Lil Wayne kumshukuru kwa kumfanya baba kwa mara ya nne.

Hata hivyo, Nivea, ambaye ana watoto wengine watatu kutoka aliowapata wakati wa uhusiano wake na Produza zamani wa muziki Dream, amewataka mashabiki wake kumuombea ajifungue salama ili aweze kurudi kwenye game kama kawaida

Kwa Lili Wayne kama mtoto huyu atazaliwa salama basi atakuwa ni mtoto wake wa pili kuzaliwa kwa mwaka huu pekee kwani hivi karibuni mwanamitindo maarufu Lauren London alijifungua mtoto mwingine wa nyota huyu wa songi la Lolipop mnamo September na kumpa jina la Lennox Samuel Ari . sambamba na watotio wake wa awali Dwayne Carter III, na pia , Reginae, aliyemzaa na mke wake wa zamani Antonia Carter.

TAFUTA HAPA

UNGANA NASI

Delicious Digg Facebook Favorites More Stumbleupon Twitter